Kweli ya Leo
Usigeuke kwa kuume wala kwa kushoto; Ondoa mguu wako maovuni (Mithali 4:27 )
Rafiki kwa Rafiki
Wakati wa mwisho wa ibada, muumini mmoja alitoka mbele na kumfuata mtumishi wa Mungu ili kuongea naye. Alikuwa amechukizwa sana na dhambi za maisha yake na dharau isiyo na kifani kwa Mungu wake. Akiwa na machozi yanamtiririka usoni mwake mtu yule mwenye kujutia alichukua mkono wa mtumishi wa Mungu na kuanza kuungama na kujutia dhambi zake kuwa uhai wake ulijaa dhambi tupu, lakini kilichosikika ni kuwa “Dhambi zangu zimejaa uhai”
Sijui kuhusu wewe, lakini mimi dhambi zangu “zina uhai” Mara kwa mara nashangazwa lakini pia nasikitishwa na watu wanaodhania kuwa kwa sababu tu mimi nimeokoka na nimempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yangu basi mimi ni mtakatifu zaidi yao, au ni bora kuliko wao au sipambani na dhambi kama wao wanavyopambana. Uliza mume wangu, watoto na familia yangu kwa ujumla, watakueleza magumu ya kibinadamu ninayopitia. Ninashukuru kuwa mbwa na kuku wa nyumbani kwetu hawawezi kuongea hali halisi. Kwa kuwa ninaishi kwenye ulimwengu huu dhaifu wenye heka heka na dhambi kibao ni lazima nipambane na dhambi kama binadamu mwingine yeyote.
Hata hivyo, nimebuni mbinu mbali mbali za kushughulika na dhambi zangu katika ulimwengu huu wenye dhambi ya asili. Mbinu ya kwanza ni kuainisha/ kulinganisha ni mfumo ninaoupendelea zaidi. Kulinganisha dhambi zangu na za mwingine, lakini pia mbinu nyingine niipendayo ni “kuzizika na kuamini kamwe hazitarudia” Hakika ni kuwa hakuna kinachosafisha dhambi zaidi ya damu ya Yesu Kristo
Tunapoyaelekezea maisha yetu kwa Mungu, yeye huiweka miguu yetu kwenye njia iliyo sahihi. Lakini ili kuendelea kuwa kwenye hiyo njia sahihi tunahitajika kuendelea kuzikataa dhambi na kuzikimbia kabisa. Kwa kuwa na chaguo lisilo sahihi tunafuata njia za pembeni na njia za mkato na kujikuta tumeingia kwenye njia isiyo sahihi na kuelekea mahali pasipo sahihi. Suleimani anatuonya tusigeuzie miguu yetu maovuni (Mithali 4:27) Tunapoziona dhambi au upenyo wa kufanya dhambi tunatakiwa kugeuka nyuma na kukimbia kulekea mueleko tofauti kabisa. Tunatakiwa tujiondoeoe kabisa kwenye dhambi. Tunafanya nini badala yake? Tunataka kuokolewa kwenye dhambi lakini huku tunataka kuwasiliana na hizo hizo dhambi. Tunasali na kuomba “usitutie katika vishawishi” lakini kwa hiari yetu tunarudia kutenda maovu. Kwa ufahari na kiburi chetu tunadhania tunaweza kuepuka dhambi na vishawishi vya dhambi peke yetu. Kwa desturi hii ni mualiko ulio wazi kwa adui kuchukua nafasi yake kwa majigambo makubwa.
Imekuwa ni desturi kwa wanaume wengi wanapokuwa wamekaa au wanaendesha magari basi kila mwanamke atakayepita mbele yake ni lazima amuangalie tena saa nyingine ni kwa jicho la mahaba. Hapa unakuta mwanaume ameona upenyo wa kufanya dhambi na anaangalia uwezekano wa kufanya dhambi, mwanaume mwenye kumcha Mungu atakimbia na kuelekea uelekeo tofauti na kama ni hayo macho yanataka kukuponza basi ni vyema ukayanyofoa na kuyatupilia mbali kwani ni bora kukosa kiungo kimoja kuliko kuruhusu hicho kiungo kimoja kuutumbukiza mwili wote kwenye ziwa la moto Vile vile kuna kina dada ambao pamoja na kujua kuwa huyu mwanaume ni mume wa mtu basi wao huanza kuwatamanisha hao wanaume kushiriki nao vitendo viovu. (Mathayo 15:19) Maana moyoni hutoka mawazo maovu yanayosababisha uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na kashfa. Ole wenu.
Hakuna binadamu anayeishi pasipo majaribu, lakini ni hiari yetu kwenda mbele au kurudi nyuma, kutakaswa au kijiangamiza. Wapendwa msikate tamaa wala msirudi nyuma msije mkamjengea himaya adui shetani (dhambi). Kataeni dhambi, kimbieni dhambi , dhambi ni mbaya, dhambi inaua na mshahara wa dhambi ni MAUTI
Tuombe
Baba unisamehe kwa dhambi za maisha yangu. Toka sasa ninaamua kuzikataa dhambi, nakugeukia wewe Bwana. Ninajua kuwa nimepotea na sina msaada zaidi yako Baba, ninatambua maisha yangu bila wewe ni bure tu. Ahsante kwa wema na fadhili zako zisizokuwa na kikomo ahsante kwa kunisamehe bila kuchoka. Katika jina la Yesu ninaomba na kushukuru
Amen
Sasa ni wakati wako
Soma 1 Wakorintho 10:13 Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.
Ukizingatia ahadi zilizopo kwenye mstari huo wa 1 Wakorintho 10:13 ahadi hizo zina maana gain kwani kwako na zinatendaje katika maisha yako?
Ø Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu.
Ø Mungu ni mwaminifu
Ø Hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu
Ø Atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.
No comments:
Post a Comment