Hivi jamani mnajua jukumu la kutunza wazee wetu ni letu sote? Huwa inaniuma sana kuona vizee hasa huko vijijini havina matunzo vinakula kwa kubangaiza, vinalala kwenye nyumba zisizo bora huku watoto na wajukuu wao wapo mjini wanaishi vizuri tena kifahari kabisa. Hebu tujiulize ni wangapi mnawatunza wazee wenu?
Bibi yangu alikuwa anapewa matunzo ya hali ya juu, nadhani aliwajengea hiyo desturi wanawe. Ilikuwa wamama na wajomba zetu ni lazima wachangishane kwa ajili ya matunzo ya bibi "mdala" hivyo ndivyo alivyokuwa akitambulika. Walikuwa wanachangishana hela kwa ajili ya chakula kile ambacho hajakilima (mchele, ngano nk) hela kwa ajili ya kilimo, maana alikuwa hauzi mazao yake; alikuwa akivuna anaanza kugawa kwa watoto na wajukuu, hela kwa ajili ya wasaidizi wake wa mashambani na nyumbani.
Ninaamini bibi yangu alifariki akijua alikuwa anapendwa na aliowaacha nyuma na alikufa akiwa na amani. PUMZIKA KWA AMANI MDALA RODA MWAKA
No comments:
Post a Comment