Wednesday, 23 May 2012

Hivi Inawezekanaje?

Wapendwa wangu wasomaji, nimekuwa mara kwa mara najiuliza haya maswali na sipati majibu;-

  1. Hivi inawezekanaje ukampenda Mungu usiyemuona na kumchukia jirani, mke, au hata mwanadamu yeyote unayemuona?
  2. Hivi inawezekanaje ukasamehewa ilihali wewe huwezi kusamehe wenzako?
  3. Hivi inawezekananje ukampiga/kumtesa mkeo ilihali imeandikwa mtakuwa mwili mmoja?
  4. Hivi inawezekanaje ukaona watu wote wabaya isipokuwa wewe tu?
  5. Hivi inawezekanaje ukataka kutendewa mema wakati wewe hutendei wenzako mema?
  6. Hivi inawezekanaje ukasaidia watu wa mbali wakati wa familia yako wanateseka? Ni umaarufu ama?
  7. Hivi inawezekanaje ukashangaa tabia za mwanao wakati ndivyo ulivyomlea?
  8. Hivi inawezekanaje ukajua mambo ya wenzako na yakwako yasijulikane?



No comments:

Post a Comment