Thursday, 19 May 2011

JINSI YA KUFURAHIA FAMILIA YAKO

Sehemu ya 1
Kweli ya leo
Moyo wa mumewe wamwamini wala hatakosa kupata mapato. Humtendea mema wala si mabaya siku zote za maisha yake . Bali mwanamke amchaye BWANA ndiye atakayesifiwa. (Mithali 31:11-12, 30)



Rafiki kwa Rafiki
Familia ina maana tofauti kwa watu tofauti. Familia ni nini? Nitakwambia ukweli kuwa si kama ilivyokuwa zamani, familia ya kisasa si rahisi, ina utata na inabadilika mara kwa mara na ni mchanganyiko wa mahusiano tofauti.
Ø     Wanandoa wenye watoto
Ø     Wanandoa wasiokuwa na watoto
Ø     Wanawake wapweke wenye watoto
Ø     Wanaume wapweke wenye watoto
Ø     Babu na bibi wenye watoto
Ø     Wazazi wenye watoto wakubwa ambao waliondoka na kurudi tena nyumbani
Ø     Marafiki wa karibu wanaoishi pamoja
Ø     Watu wa aina mbali mbali wanaoishi pamoja
Wote hao ni familia. Familia ni kikundi cha watu kinachoishi pamoja. Kitu kilicho cha muhimu kuliko tafsiri ya neon familia lenyewe ni nia na lengo la familia. Hakuna familia iliyo kamilifu. Haijawahi kutokea na haitakaa itokee familia kamilifu hapa duniani. Hata hivyo madhumuni ya familia hapa duniani ni kudhihirisha  uhalisia na uwepo wa Mungu hapa duniani, kwa lugha nyingine ni kwamba “familia ni sehemu ya msingi tunayoweza kujifunza juu ya Mungu.
Katika darasa moja la shule ya Jumapili (Sunday school) watoto waliamriwa kuchora picha ya Mungu. Mwalimu alipopita kukagua hizo kazi za kuchora picha ya Mungu, watoto walikuwa na shauku ya kumuonyesha michoro yao. Mtoto mmoja alimchora Mungu katika mfumo wa Mwanga mkali wa “upinde wa mvua” (rainbow).

Mwingine alichora taswira ya mwanaume mzee akitoka katika mawingu mazito.

 na kuna mmoja alichora mchoro uliofanana na “superman” (sijui kwa Kiswahili) (mwanaumebora???)

Inawezekana mchoro bora ulitoka kwa binti mmoja aliyesema “sijaweza kujua Mungu anafananaje hasa kwa hiyo nimemchora baba yangu”

Familia ni muhimu kwa Mungu. Mungu alitengeneza familia kabla hajatengeneza kanisa na ana mpango familia iwe ni yenye mafanikio. Na katika kiini cha huo mpango wa mafanikio ya familia kuna UPENDO. Ili kuwa sehemu ya familia unatakiwa kupenda na kupendwa. Changamoto kubwa hapa ni jinsi gani tunaweza kuzipenda familia zetu?
Ninajua kuwa wote tunataka kuwa sehemu ya familia ambapo tunatoa na kupokea upendo. Mithali 31 inatueleza ni kwa jinsi gani. Katika sura hii taswira/ sura ya mwanamke, mke na mama imechorwa na mfalme kama aina ya mwanamke ambaye mama anataka kijana wake amuoe. Ni mwanamke wa kiwango cha juu cha ubora siyo tu kwa wanawake bali kwa kila mwana familia. Katika maisha ya huyu mwanamke tunakutana njia tofauti za kupenda familia zetu.

Jenga uaminifu
(Mithali 31:11) inatuambia “Moyo wa mumewe humuamini” “humuamini” ni kumlinda na kumtumainia. Mwanamke wa Mithali 31 aliishi maisha yake yote akijenga uaminifu. Alimuamini Mungu na kuwa na uhusiano binafsi na Mungu. Hatuwezi kuaminika kama hatuamini na kama hatumuamini Mungu, hatuwezi kuwaamini wengine. Na kama hatuwezi kumuamini Yesu Kristo au kumtumaini yeye wakati wengine wanatuamini na kututumainia hakika hatutafanikiwa kwani tutaanguka. Uaminifu huondoa hofu!!
 (Zaburi 56:3-5) “Siku ya hofu yangu nitakutumainia wewe, kwa msaada wa Mungu nitalisifu neno lake. Nimemtumaini Mungu sitaogopa; mwenye mwili atanitenda nini?” Uaminifu ni kitu rahisi kuharibika, na ukiharibika si rahisi sana kuurejesha kama ulivyokuwa hapo awali.
Ili kufurahia familia zetu tunatakiwa kwanza tumuamini Mungu kabla hatujaziamini familia zetu. Familia zetu zinatakiwa ziweze kutuamini sisi kwa hali yeyote ile bila kuwa na shaka kabisa. Kutakuwa hakuna furaha kwenye familia zetu kama hakuna mazingira ya uaminifu au kuaminiana. Familia ni kama “timu” na hakuna kitu hatarishi kinachoweza kuuwa timu kama kukosa kuaminiana. Muamini Mungu halafu jenga uamninfu kwa familia yako.

Tuombe
Baba, nakushukuru kwa familia ulionijalia. Nataka kuwapenda kama wanavyohitaji kupendwa. Nisaidie kujenga uaminifu kwao kama wanavyojifunza kukuamini wewe zaidi. Bwana nisaidie niwe mwaminifu na niwe mwanamke unayependezwa naye.
Ninayaomba haya katika Kristo Bwana na mwombezi wetu.
Amen
Sasa ni zamu yako
Ø Tengeneza orodha ya njia za jinsi ya familia yako kukuweza kukuamini na kukuaminia
Ø Ainisha maeneo unayodhani unatakiwa kujenga uaminifu zaidi
Ø  Mara kadhaa angalia njia inayoweza kuwakumbusha wanafamilia yako kuwa ninyi ni timu moja
Ø  Kuwa na kikao cha familia kuzungumzia ina maanisha nini kuwa timu moja.

Kwa mtazamo wangu
Kila mahali ninapoangalia nakutana na familia zenye “nyufa” au zilizo “bomoka”. Kwanini??? Ninaamini kuna sehemu uaminifu unavunjika kwa kuwa na mahusiano au usaliti au kwa wanafamilia kusahau viapo vyao.  Kinachotisha zaidi ni pale inapochukuliwa kuwa ni kawaida kuvunjika kwa uaminifu. Mungu anatuita na kutusihi tumuamini na tujenge uaminifu kwenye familia zetu. Haijalishi ni mara ngapi umejaribu bila mafanikio kujenga uaminifu kwa familia yako, anza sasa na Mungu atakusaidia ukimuamini kuwa atakuwezesha kujenga uaminifu kwa familia yako.


Ahsanteni, na subirieni sehemu ya 2 ya "Jinsi ya Kufurahia Familia Yako".

No comments:

Post a Comment