Thursday, 15 September 2011

Jinsi ya kumjua MUNGU

Je unajua inakugharimu nini kuwa na uhusiano mzuri na Mungu wako? Jikane mwenyewe uwe mtu mwema ili Mungu akukubali. Mungu ameweka wazi kwenye maandiko matakatifu (BIBLIA) jinsi ya kumjua yeye na kumtumikia. Zifuatazo ni kanuni zitakuelekeza jinsi gani unaweza kumjua Mungu kwa kupitia mwanawe mpendwa Yesu Kristo

1. Mungu anakupenda na ana mpango mzuri kwa maisha yako.

Upendo wa Mungu
  • "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele" (Yohana 3:16)
Mpango wa Mungu
  • Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. (Yohana 10:10)
2. Sisi sote ni watenda dhambi na dhambi zetu ndizo zinazotutenga na Mungu

Watenda dhambi
  • kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (Warumi 3:23)
  • Tuliumbwa ili tuwe na uhusiano mzuri na Mungu lakini kwa kiburi chetu tuliamua kuzifuata njia zetu wenyewe na hapo ndipo uhusiano wetu na Mungu ulipovunjika
Tumejitenga na Mungu
  • Warumi 6:23 yasema, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti
Mauti ya milele ndiyo tunayopokea kama mshahara wa dhambi zetu. Mauti ya "kiroho" ndiyo tunayoizungumzia hapa yaani kujitenga na MUNGU.

3. Yesu Kristo ndiyo njia pekee ya kutufikisha mbinguni, kwa yeye tunaweza kuona mapenzi ya Mungu na mipange yake juu ya maisha yetu.

Alikufa kwa ajili yetu

Alifufuka kwa ajili yetu
  • Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu....... Alizikwa.......... Siku ya tatu akafufuka kama yanenavyo maandiko matakatifu, alimtokea/ kujidhihilisha kwa Petro, wanafunzi wake 12 na kwa makundi ya watu.

Yesu ndiye njia pekee kwenda kwa Mungu

4. Inatupasa kumpokea Kristo kuwa Bwana na Mwokozi ndipo tutakapojua pendo na mipango ya Mungu kwa maisha yetu.

Ni lazima tumpokee Kristo
  • Lakini wale wote waliompokea na kumwamini, hao aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu. (Yohana 1:12)

Tunampokea Yesu kwa Imani
  • Maana, kwa neema ya Mungu mmekombolewa kwa njia ya imani. Jambo hili si matokeo ya juhudi  zenu, bali ni zawadi ya Mungu (Waefeso 2:8)

Tunapompokea Yesu, tunazaliwa upya
  • Yesu anatuita "Sikiliza! Mimi nasimama mlangoni na kubisha hodi. Mtu akisikia sauti yangu na kufungua mlango, nitaingia nyumbani kwake na kula chakula pamoja naye, naye atakula pamoja nami" (Ufunuo 3:20)

  • Kumpokea Yesu ni kumgeukia Mungu yaani "kujikana mwenyewe"  na kumwamini Kristo kumfanya kuwa sehemu ya maisha yetu na kutufanya kuwa wana wake. Inatupasa kumkaribisha Yesu maishani mwetu yeye atuongoze katika maisha yetu.

Unaweza kumpokea Kristo sasa kwa imani kwa njia ya Sala/ Maombi
Sala ni kuongea na Mungu. Mungu anakujua na kujua kila hitaji lako haijalishi hata kama hujui kupanga maneno ya sala vizuri.

(Hii ni sala ninayoipendekeza mimi)
Bwana Yesu, nakuhitaji. Ahsante kwa kufa kwako msalabani kwa ajili ya dhambi zangu.  Ninafungua mlango wa moyo wangu ili uingie nami nikupokee kama Bwana na Mwokozi wangu. Asante kwa kunisamehe dhambi zangu na kunipa uzima wa milele. Tawala maisha yangu eeh Bwana. Nifanye kuwa vile upendavyo mimi niwe. Katika Kristo ninaomba na kushukuru Amen.

No comments:

Post a Comment