Tuesday, 20 September 2011

Umnyonge?? Usihofu bado una THAMANI mbele za Mungu

Mpendwa, je unahisi thamani yako imeshuka? Watu wanakucheka, wanakudharau? Usihofu kwa Mungu wewe bado una THAMANI kubwa.

2 Wakorintho 4:7
Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu.

Kulikuwa na mkusanyiko wa watu wengi mahala fulani basi yule aliyekuwa kiongozi wa ule mkusanyiko akainua hundi juu hundi iliyokuwa na thamani kubwa ya pesa; na kuuliza umati uliokusanyika, "je kuna anayeitaka hii hundi??? Watu wote wakanyoosha mikono kuashiria kuwa wanaitaka. Yule kiongozi akaikunja kunja ile hundi na akaitupa chini ile hundi na kuikanyaga halafu akaiinua tena na kusema "haya sasa anaiyetaka anyooshe mkono" mikono yote tena ikainuliwa juu. Je unajua ni kwanini watu wote waliinua mikono yao juu???

Hiyo ndiyo sababu MUNGU bado anakuhitaji!!! Unaweza kuwa umepondeka pondeka, una michubuko, na umesinyaa lakini bado vyoete hivyo havibadilishi THAMANI yako kwa Mungu wetu kama ambavyo hundi ile bado inathamani pamoja na kujikunja na kuchafuka kwake lakini bado watu walikuwa wanaitaka.

Bado una thamani kubwa kwa Mungu na bado Mungu anakupenda na ndio maana akakuchagua na kukubadilisha kuwa ulivyo.

Mungu anatujua tulivyo na anajua kuwa sisi ni mavumbi (Zab 103:14)  Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi. Mungu anajua kuwa sisi ni viumbe dhaifu sana.


SALA YA LEO
Mwenyezi Mungu japokuwa nimedharauliwa, nimechekwa, nimetengwa najua bado nina thamani kubwa kwako. Ahsante kwa kunipenda hata kumtoa mwanao wa mpendwa Yesu, kufa kwa jili ya dhambi zangu. Ahsante kwa kuniandalia njia ya uzima wa milele kupitia kupigwa na kuteswa kwa Yesu Kristo. Ahsante kwa kuniona mimi ni hazina kubwa kwako.
Ninaomba na kushukuru katika Kristo Yesu

Amen.

KAZI KWAKO
Je umeupenda mfano wa hundi iliyofinyangwa, kukanyagwa na kuchafuliwa? Leo unaweza kutumia mfano huo kwa rafiki au mtoto ambaye amenyong'onyezwa kimaisha na rafiki yake. Inaweza kumsaidia JARIBU!!!

No comments:

Post a Comment