1. Kupata hela
2. Kuwa na sikukuu katikati ya week (siku za kazi)
3. Kulala kwenye mashuka fresh kitandani kwako (hasa wanaume wanapenda hii)
4. Kuogelea (Kama siyo muoga
5. Kusikia neno nakupenda kutoka kwa umpendaye
6. Kupumzika kwenye kijua cha asubuhi (ambacho siyo kikali
7. Kupokea
8. Kupata ujumbe (sms) za mahaba kutoka kwa umpendaye
9. Kukumbatiwa (pale unapojisikia)
10. Kutumiwa ujumbe/ kadi ya shukrani kutoka kwa mtu uliyemsaidia
11. Kuwaona wazee (Bi/ Bw.) wameshikana mikono (unatamani ingekuwa wewe na umpendaye)
12. Kuendesha gari huku unasikiliza muziki kwa sauti ya juu kidogo
13. Kushinda bahati nasibu hata kama ni ya Tsh. 20,000/= (
14. Kupanga mambo ya likizo (hasa ya mwisho wa mwaka)
15. Kusikiliza muziki unaoupenda
16. Kupata kitu kwa bei ya punguzo
17. Kukutana ra rafiki wa zamani hasa utotoni (Ooh hii naipenda
19. Kupandishwa cheo kazini (Haaa haaa hasa mshahara ukipanda lol)
20. Kwenda matembezi ya jioni na umpendaye (Dinner for two i real like it)
21. Kusikiliza muziki ambao utakukumbusha mambo yako ya zamani (Mi huwa nikisikiliza Mwanameka na Mayasa duh sisemi)
22. Kuangalia picha za zamani (Nina picha yangu nikiwa some months old naipenda
Baby me haaaa haaaaa
24. Kuwa na muda wako binafsi (ukitaka kulala hayaa.. ukitaka kucheza hayaa bora ni wewe peke yako)
25. Kuwa mzazi mtarajiwa (Mimi kuwa na mimba napenda
26. Kusikia ki/vicheko vya watoto (hasa wakiwa watoto wako)
27. Kuwa na usiku wa wadada/ wakaka kutoka peke
28. Kuamka asubuhi na kugundua kuwa ni Jumamosi (Yuhuuuuuu its Saturday)
29. Kunywa kitu unachokipenda sanaaa ( Kwangu mimi ni Fanta ya baridi)
30. Kula kitu unachokipenda
31. Kuweza kuvaa jeans ambayo hapo awali haikuwa ikikutosha (Hasa kama umepungua unene lol)
32. Kusifiwa na mkuu wako wa kazi (Boss)
33. Kusikia harufu nzuri ya mikate na keki inayookwa (Pita shoprite kule bakery utajua)
34. Kufanya pedicure (Hasa kupata ile massage aahaaa i like it)
35. Mtu kukwambia kuwa umepungua uzito (Heee heee niulizeni ninavyopata bichwa nikiambiwa hivyo)
36. Kugundua kuwa kuna mtu anapenda
37. Kwenda sinema ukiwa na umpendaye au company ya nguvu
38. Kurudi kwa umeme hasa
39. Kufika mwisho wa safari kama unaenda mapumziko (
Malaika Beach Resort - Mwanza
40. Kutengeneza nywele hadi ujihisi umependeza (Inakujengea ujasiri wa hali ya juu)
41. Kukuta bank account yako ina hela (hata
42. Kupata leseni ya udereva/ Passport
43. Kukaa kwenye hoteli ya kifahari
44. Kuambiwa na wanao kuwa wanafanya vizuri darasana (na hasa ikija report ya shule)
45. Upo kwenye daladala umesimama umechoka halafu abiria uliyesimama pembeni yake awe anashuka kwa hiyo wewe unapata nafasi
46. Mtu kukurushia muda wa maongezi (Tigo rusha, Voda fast. Airtel................. )
47. Kulala huku kuna kamvua kananyesha na ka-ubaridi kwa mbali
48. Kupata kinywaji cha baridi baada ya kumaliza kazi (Juice, Soda, beer and Wine)
49. Kuwa muumini mzuri wa dini yako
My Bible School Certificate na bado naendelea...... God bless me!!!
Wewe unafikiri nini juu ya hii list? kuna chochote kilichopungua unadhani kingekuwepo?
No comments:
Post a Comment