Monday, 28 November 2011

Mlimani City hiyooooooooo

 Hiki ni choo namba 3 kinafanya kazi lakini hali yake ya usafi ndio kama hivyo... Hairidhishi hata kidogo

 Katika vyumba 6 au 7 vya vyoo ni 2 tu ndio vinatumika vingine vimefungwa

 Hiki kimekuwa stoo ya vifaa vya usafi japo wasafishaji wenyewe hawapo tena
 Hapa limewekwa dustbin maana yake "usithubutu" kufunua na ukifinua "at your own risk"
 Hiki kimefungwa, nadhani aliyefunga alifunga kwa ndani alipomaliza akarukia upande wa pili
 Hapo kwenye kibaraza cheusi, palipotupwa hayo makaratasi ndipo walipokuwa wanakaa watu wa usafi lakini kwa sasa hakuna mtoa huduma ya usafi
Milango imeharibika kama mara 4 hivi na hayo ndio marekebisho yake
Jamani are we serious kweli eti hapa hapajamaliza hata miaka 10 toka paanze kutumika lakini pamezeeka ile mbaya sasa sijui wa kulaumia ni sisi watumiaji au wenyewe wanaohudumia jengo? Fungukeni!!!!

1 comment:

  1. Tupo pamoja ndugu yangu, nashukuru kuwa umejiunga nami ndugu yangu, ubarikiwe sana

    ReplyDelete