Mungu nisaidie ili niwe mke mwema
kwa mume wangu, Ninajua fika siwezi kuwa mke mwema bila wewe kuhusika kunifanya
kuwa hivyo.
Ondosha ubinafsi wangu, makwazo yangu, na
kukata kwangu tama na ubadilishe kuwa uvumilivu na utayari wa kuyakubali yote.
Ondosha tabia zangu za hasira,
hisia, kujihami na unifanye mwenye uvumilivu, huruma, mwema, mwaminifu, mpole
na mwenye kujiamini
Ondosha ugumu wa moyo wangu na
uvunje kuta za kuteseka kwangu. Uniumbie moyo safi na uniwekee mapenzi, amani
na furaha ndani yake.
Najua peke yangu siwezi baba ila
ni kwa msaada wako tu.
Nionyeshe dhambi zangu zinapojidhihirisha moyoni mwangu na hasa pale inapomuhusu mume wangu mpenzi. Ninakiri kuna wakati sikuwa na mapenzi naye, nikiwa na chuki naye, hasira naye na hata kumdharau na kutomjalikama mume wangu
na kutomsamehe kwa pale aliponikosea.
Nionyeshe dhambi zangu zinapojidhihirisha moyoni mwangu na hasa pale inapomuhusu mume wangu mpenzi. Ninakiri kuna wakati sikuwa na mapenzi naye, nikiwa na chuki naye, hasira naye na hata kumdharau na kutomjali
Baba naomba uniponye maumivu ya
moyo wangu pale nilipoumizwa na mume wangu, uzipoze hasira zangu na unipe
ujasiri pale nilipokata tama na unisaidie kumsamehe hata kama hajaniomba
msamaha kama wewe unavyonisamehe na kamwe huwa
hukumbuki maovu yangu.
Baba nakuomba unifanye mimi kuwa
chombo cha suluhu, amani na uponyaji wa ndoa yangu na mume wangu.
Baba naomba utusaidie mimi na mume
wangu tuweze kuwasiliana vizuri na kuepukana na pepo wa kutengana anapojisogeza
kati yetu. Mfanye mume wangu kuwa mwenzangu, rafiki yangu, kiongozi wangu, baba
wa watoto wangu na msaada wangu na kwa familia yetu kwa ujumla.
Nisaidie niweze kutengeneza mazingira mazuri
ya amani, furaha, salama na upendo ili hata yeye atamani kurudi nyumbani na
kukutana na hayo mambo mazuri.
Baba nakuomba unifundishe jinsi ya
kujitunza ili niweze kuendelea kuwa na mvuto kwake kama
mke.
Ee baba unikuze niwe mwanamke
mbunifu na mwenye kujiamini ambaye nitakuwa tajiri wa fikra, akili, roho na
moyo. Nifanye niwe mwanamke ambaye mume wangu atajisikia ufahari kusema mimi ni
“mke wake” mbele ya wenzake.
Baba nayaweka matarajio na maombi yangu yote msalabani ili ukashughulike nayo.
Ninamuachia mume wangu kutoka
kwenye mzigo wa kwa kunitimizia yale niliyofikiria ni yeye pekee anaweza
kuyatimiza nakuletea wewe baba ili unitimizie
Unisaidie kumkubali jinsi alivyo
na wala si kumbadilisha, nimegundua kuwa kwa kiasi fulani hawezi kubadilia
lakini pia kwa wakati huo huo nakukabidhi umbadilishe kwa kadri ya upendavyo
wewe kwa kiasi ambacho sijawahi kufikiria anaweza kubadilika.
Ninaacha mikononi mwako mabadiliko
yoyote utakayoona wewe yampasa kubadilika, ninamkubali vyovyote alivyo kwani
hakuna aliye mkamilifu kati yetu bali wewe BWANA usiyebadilika ndiye mkamilifu
na nina imani utatufanya sisi kuwa wakamilifu kadri ya mapenzi yako.
Baba ninaomba unifundishe jinsi ya
kuomba kwa ajili ya mume wangu na ufanye maombi yangu kuwa lugha sahihi ya
mapenzi yetu.
Pale mapenzi yalipokosa nguvu baba
tengeneza upya mapenzi kati yetu. Nionyeshe mapenzi ya kweli yalivyo na jinsi
ya kuwasiliana naye ili naye aweze kunielewa.
Jenga umoja na mshikamano kati
yetu ili tuweze kukubaliana kwa kila jambo. Mungu wa uvumilivu, Mungu wa
ustahamilivu na Mungu wa Faraja utajalie mawazo yetu yawe sahihi kwa kila mmoja
kwa jina jina la Yesu.
Utufanye sisi kuwa wamoja wala
usitutenge, usitufanye washindani, usitufanye kila mtu ashike lake bali
utufanye kuwa wamoja, tusihesabiane madhaifu ya kila mmoja wetu wala makosa
yake ili tuwe na mahusiano yenye upendo na amani.
Utusaidie baba tujadili kwa amani
yale yenye maana na kutujenga tu; kwa yale yenye kuumiza na kuturudisha nyuma
baba tunaomba uyaondoshe kwetu.
Baba ninaomba viapo vyetu kwa kila mmoja wetu vizidi kustawi na mapenzi yazidi kuongezeka siku hadi siku..
Msaidie mume wangu awe ndio
kiongozi na kichwa cha familia yetu kama
ulivyomfanya kuwa toka kwenye ile bustani ya Eden. Baba uniwezeshe niweze
kumsaidia, kumuwezesha na kumuheshimu. Niwezeshe
kuelewa ndoto zake na matamanio yake kadri anavyotamani kuwa. Nionyeshe matakwa
yake na mahitaji yake na pia unionyeshe kabla hayajajitokeza ili niwe na
suluhisho. Baba rudishsha uhai kwenye
ndoa hii wala isiteteleke tena.
Baba unifanye mtu mpya, baba unipe
mtazamo mpya, na mtazamo chanya na uhusiano ulio imara na mwanaume uliyenipa.
Nisaidie nimuone kwa jicho jipya, mapenzi mapya na kumkubali upya.
Mpe mume wangu MKE MPYA na mke
huyo awe ni mimi Lulu na si wala mwingine.
Ninaomba haya katika Kristo Bwana na Mwokozi wetu AMEN
…………….....................................................………………………………
Nimeipenda hii sala. Naomba kupokea mafundisho mengine yahusuyo ndoa kama yapo. Ahsante!
ReplyDeleteamen
DeleteMungu tusaidiane sisi wanawake tulio ndoan upokee sala za unyonge wetu
ReplyDeleteSala nzuri,barikiwa sana
ReplyDeletei love it... nimeisoma na hisia zote kama mm ndio ninayoiomba asante mtoa maombi haya
ReplyDeleteBe blessed
ReplyDeleteAmen, sala nzuri sana ina leta hisia na uhalisia wa kweli, be blessed
ReplyDeleteAmen Asante kwa sala
ReplyDeleteAmen na naamini imekuwa kama nilivyoomba asante Yesu
ReplyDeleteNa ikawe hivi kwa Jina la.Yesu
ReplyDelete