Mimi ni mzazi mwenye binti wa umri unakaribiana na wa binti "Lulu" Elizabeth Michael.
Mara nyingi tunawakanya watoto wetu wasifanye mambo fulani kwa kujua kuwa kwa umri wao si mazuri lakini pia kutokana na kiburi cha "umri" huo huo huwa wanadharau na saa zingine kutuona "wanoko". Ninaamini Lulu amekanywa mara kadhaa juu ya mwenendo wake lakini hakusikia, inawezekana alikanywa na wazazi wake, majirani, jamii au hata wapenzi wake wa filamu zake ikiwemo mimi binafsi. Nimewahi kuwa na mawasiliano naye kwenye facebook na kumpa feedback za tabia zake na madhara yake lakini kamwe hakujirekebisha.
Ninaamini kilichomtokea ni bahati mbaya ambayo hata mimi na wewe inaweza kutukuta ila kwa kuwa yeye alikuwa na "kiranga" basi watu watamchukia mara dufu!! Ni imani yangu kuwa hakuwa na dhamira au lengo la kumuua huyo mpenzi wake wa siri ambaye kwa umri hakustahili kuwa mpenzi wake lakini pia kimaadili haikuwa sahihi.
Namuonea huruma lakini pia naona itakuwa ni fundisho kwa watoto wetu wenye umri huo kuwa wasiposikiliza maneno ya wakubwa wao basi ipo siku watakuwa matatizoni kwa njia moja au nyingine.
Iliyobaki LULU ni kumrudia muumba wako, na wazazi wako wanatakiwa kufunga na kusali ili angalau uepuke hukumu ya kunyongwa hadi kufa kwa kesi ya kuua kwa kukusudia ni bora iwe kuuwa bila kukusudia.
KANUMBA upumzike kwa amani na Mungu akuhukumu kadri ya matendo yako - kwani siamini kuwa tunaweza kukuombea Mungu akusamehe maovu yako kwani muda wa kuomba msamaha ulikuwa nao hivyo kama hukuutumia ndio bahati mbaya tena!!!
No comments:
Post a Comment