Unafahamu kutokusamehe kunafanya usipokee muujiza wako? Hakika! unajifungia baraka zako, maana ndani ya moyo wako umejaa uchungu na kuumizwa. Je umemkwaza/kukwazwa mtu na kila ukumbukapo unaumia na kuwaza mabaya juu yake?
Ndio maana maombi yako hayajibiwi! sasa ebu angalia moyoni mwako umemuweka nani! MSAMEHE na uombe REHEMA kwako na kwake na USAHAU kabisa! Ikibidi mfuate mwambie UMEMSAMEHE.
Utakuwa huru, umefunguliwa! utamuita Mungu naye atakuitikia, utapokea yale Mungu amekusudia kwako Isaya 43:26 Unikumbushe, na tuhojiane, eleza mambo yako, upate kupewa haki yako”
KUSAMEHE KUNAFUNGUA VIFUNGO
No comments:
Post a Comment