
Ha ha ha ha ha. Kicheko kina raha yake bwana au vipi? Hivi karibuni wana-sayansi wamebaini kuwa kicheko cha dakika 1 kinaweza kuongeza ufanisi kwenye mfumo wako wa kinga za mwili kwa masaa takribani 24, lakini hasira yako ya saa 1 inaweza kuvuruga huo mfumo kwa masaa 6 au zaidi. Heeee heeee heeee!!! Naamini unajisikia kucheka zaidi sasa……. Uongo uongo??? Kweliiiiiii (sauti ya mashauzi ya kitaarab)

Lakini kuna wakati maisha na mashaka ya maisha huiba vicheko vyetu. Kumbuka ilivyokuwa rahisi ulipokuwa mtoto kucheka kwa kila jambo hata
Mungu anawacheka adui zake hivyo hata nasi tunaweza pia. Zaburi 2:4 Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka. Hapa tunaona jinsi mwenendo wa Mungu juu ya adui zake ulivyo. Hivi umeshawahi kutafakari taswira ya Mungu akicheka? Lazima ni taswira nzuri na ya ajabu. Mara nyingi tunakuwa na taswira ya Mungu akiwa amekasirishwa na matendo yetu maovu lakini hiyo siyo mwisho kwani pamoja na kuwa Mungu hukasirishwa na maovu yetu lakini pia hufurahi kwa kuwa hujua hatima yetu kwani huuona mwisho wetu kuanzia mwanzo. Anajua kuwa ameandaa makao matakatifu kwa ajili yetu na adui zake wote wataangamia Ufunuo 7:17 unasema Kwa sababu Mwanakondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, kutawala juu
Chukua Muda Kumshukuru Mungu. Unaweza kuanza kwa kuyacheka matatizo yako kwanza kwa sababu si muda mrefu yatafikia mwisho. Muombe Mungu akupe muongozo kwani yeye ana mpango mzuri na maisha yako hivyo hofu, mashaka, shida na masumbufu yote ya sasa yataisha nawe utakuwa unayacheka yale yote yanayojitokeza kwani utakuwa unayajua mwisho wake.

No comments:
Post a Comment